KITUO CHA SHERIA BLOG
Legal Chronicles
HAKI ZA MFANYIKAZI WA KENYA NI WAJIBU WETU
UncategorizedMarch 24, 20152 CommentsKituo Cha Sheria
Kwa kipindi cha miaka mingi, Kituo cha Sheria wamepokea malalamishi mengi kutoka kwa wafanyakazi kuhusiana na kanuni na masharti ya uajiri.
Tumeona kuwa mfanyakazi Mwanakenya wa kawaida anakosa ufahamu kuhusiana na haki zake kama mfanyakazi. Tumeona vilevile kuwa waajiri wengi vilevile hawafahamu majukumu yao kwa wafanyakazi wao.
Kijitabu hiki kimeundwa kwa ajili ya wafanyakazi, waajiri na pia yeyote yule ambaye anataka kufahamu na kuelewa sheria jinsi ilivyo humu Kenya kuhusiana na mahusiano ya utenda kazi.
Ni matumaini yetu kuwa kijitabu hiki kitawasaidia wafanyakazi na waajiri pia kufahamu vyema zaidi na kuzilinda haki za wafanyakazi.
Habari iliyoko kwenye kijitabu hiki imekusanywa kutoka kwa sheria za utenda kazi za 2007, ambazo zilibatili na kuchukua nafasi ya zile sheria za 2003.
Baadhi ya sheria za 2007 tangu wakati huo zimetangazwa kuwa haziandamani na Katiba, jambo ambalo linaonyeshwa kwenye ufupisho wetu.
kutambua haki yako ya uajiri ni wajibu wako. Ili kuweza kujisomea nakala yako popote ulipo bonyeza hapa . http://kituochasheria.or.ke/gallery/publications/kiswahili-publications/
KITUO TEAM
All Comments
Said
December 7, 2021
Hello. Please of the help me kuna takiri moja hapa kwetu kaloleni alien niajiri Nika mufanyia kazi mwaka moja na nusu kunilipa amekataaa jamani kweli ni haki hiyoo 0743961502
George Frank Bruno
January 24, 2022
Hello i am working in a barbershop hia in Mombasa but the employer cant accommodate me because she cant provide the necessary tools for my work. I feel uncomfortable and i want to leave.
She gave me sum amount of 150k to work for 1yr but am feeling wasted and uncomfortable with the environment.
I have worked for 7months now but i feel uncomfortable please help me.
We have no documents of any agreement, it was just verbal agreement.
0746024674
Leave A Comment